SOMO:NAMNA KIJANA ANAPASWA KUENENDA ILI ASIDHARAULIKE
NAMNA KIJANA ANAPASWA KUENENDA ILI ASIDHARAULIKE
KWANZA TUANZE NA MAANA YA KIJANA KAA UFUPI.. .
Kijana ni Mtu wa kike au wa kiume mwenye umri wa kiaka 15-45..kwa Dunia ya Leo hivyo ndivyo tunavyoweza kumuelezea kijana..
Sasa iko ivi"Biblia inamuelezea kijana kwa namna ya kipekee sana,sijajua kama wewe unaijua hii Siri,ila ni ivi kijana anahitajika sana katika kuisukuma na kuitenda kazi ya Mungu Ili isonge mbele, katika ulimwengu wa leo wanasema kijana ni taifa la kesho,, the same katika kazi ya Mungu kijana ndiye anatakiwa kuwa mstari wa mbele kuipigania injili,, ukisoma tangu agano la kale na jipya utaona,watumishi wengi wa Mungu waliitwa na Mungu wakiwa ni vijana..Musa,daudi,Daniel,Isaya,yeremia... wanafunzi wa Yesu,Paulo...okay tufanye wote,,
👉 unazani ni kwanini waliitwa wakiwa vijana,,jibu👇
waraka wa Yohana 1:14b anasema
1 Yohana 2:14b
[14] Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu.
(kwahiyo sifa ya kijana ni nguvu tena hiyo nguvu ikiambatana na Neno la Mungu aasema mmemshinda yule mwovu,,zingatia hapa kijana anasema mmemshinda sio mtamshinda..Je? wewe umemshinda mwovu...nguvu zako zimeambatan na Neno la Mungu??
tena katika mithali anasema..
Mithali 20:29a
[29]Fahari ya vijana ni nguvu zao,
...nguvu pekee ndiyo fahari ya vijana na hii nguvu ndiyo inafanya Mungu pia atamani kututumia,maana kijana ukijitambua utaingia popote na utafanya lolote kwa ajili ya kesho yako" the same katika kumtumikia Mungu, unaweza tembea kwa miguu umbali mrefu Ili tu kuisukuma injili iende,utatembea kwa mvua bila hofu...utashinda majaribu na vikwazo na ni rahisi kuvumilia dhiki na mateso na Kila aina ya maumivu,
👉Mungu alipomuita Yoshua alimwambia uwe shujaa na ujasiri na uhodari mwingi na hodari,,kwanini ni kwasababu kijana mwenye nguvu lazima ahakikishe anavitu hivyo vitatu ujasiri na uhodari na ushujaa...ndipo ataweza kutimiza yampasayo kutenda au kufanya👇
Yoshua 1:6-7
[6]Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana ni wewe utakayewarithisha watu hawa nchi hii niliyowaapia baba zao ya kwamba nitawapa.
[7]Uwe hodari tu na ushujaa mwingi, uangalie kutenda sawasawa na sheria yote aliyokuamuru Musa mtumishi wangu; usiiache, kwenda mkono wa kuume, au wa kushoto, upate kufanikiwa sana kila uendako.
👉Lakini shida ni kwa vijana sisi wa leo hatujuhi Siri ya huu ujana tulio nao,vijana wanasema wameokoka lakini hawawezi hata kumuambia mtu habari za Yesu,wanakimbia ibada za maombi,hawataki kutenda kazi ya Mungu,so sad!!,
👉Ngoja nikuambie kitu ujana ndio key point ya kesho yetu katika maisha yetu ya Kila siku..na pia ujana ndiyo msingi wa safari yetu ya kwenda mbinguni,maana hata majaribu mengi hutupata tukiwa vijana,,wazee wazinzi walianzia ujanani,walevi,wezi,wachawi,waasherati,wavuta bangi na Kila aina ya uovu chanzo ni ujana,ukiwakuta vijana wawili wa kiume wanapiga story za wanawake utalia machozi,same tu wanawake wanavyowazungumzia wanaume utalia machozi..vijana tumekuwa wa ovyo wa ovyo kabisa
👉Na sasa mwisho wa siku haya maisha ya ovyo yametufanya vijana tunadharauliwa,hatuheshimiwi hatupewi sifa sitahiki,,tumekuwa watu ovyo mbele ya macho ya jamii inayouzunguka zaidi hatuaminiki.."
Lakini leo Mimi Nina Neno kidogo la ukombozi kwa vijana sawa sawa na Neema ya Mungu katika kristo Yesu..Namna vijana tunapaswa kuenenda ili tusidharaurike au usidharaurike zaidi uheshimiwe..Maandiko yanasema👇
1 Timotheo 4:12
[12]Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.
👉 Anasema mtu asiudharau ujana wako katika usemi na mwenendo, upendo na Imani na usafi...kumbe ni ivi kudharaulika unatengeneza mwenyewe kutokana na unavyozungumza,matendo Yako,upendo wako na Imani Yako...Yes" unatengeneza wewe...hujawaona huko kwenu watu wanatamka matusi makali mbele ya umati wa watu kana kwamba ni ndizi anaulizia sokoni,,hujawaona vijana wamelewa saa tatu asubuhi mpaka unajiuliza kazi anafanya mda Gani Wala haihitaji utetezi kwamba anafanya jioni,, maana Maandiko yanaonya nyakati zote iwe asubuhi au mchana au usiku👇
(Isaya 5:11
[11]Ole wao waamkao asubuhi na mapema, wapate kufuata kileo; wakishinda sana hata usiku wa manane mpaka mvinyo imewaka kama moto ndani yao! )).
👉kwahiyo ni ivi kijana ili usidharaurike Cha kwanza ni lazma ujitambue katika kuzungumza,,mdomoni mwako unatoa maneno Gani.."" yaani hakikisha unatoa maneno mema tu na sio maovu,,yaani kijana Linda sana moyo wako na kinywa chako((Mithali 4:23
[23]Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo;
Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.))
✓✓zaidi Paulo anasema!!👇
Waefeso 4:29
[29]Neno lo lote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wanaosikia.
👉lakini ukishindwa kuyachunga maneno ya kinywa chako katika Mithali anasema
Mithali 6:2
[2]Basi umetegwa kwa maneno ya kinywa chako,
Umekamatwa kwa maneno ya kinywa chako,
(kwahiyo maneno ya kinywa chako yanaweza kukuweka karibu na jamii au kukutenga...kwahiyo chunga sana kinywa chako Yale kinayotoa zaidi moyo wako maana huko ndiko chimbuko la yote...Ili usitengwe na jamii
👉Tena zaidi kijana angalia sana mwenendo wako,vile waenenda usianguke...matendo yako yasishuhudie kinyume na jamii inavyokwenda Bali yapendeze mbele ya jamii Ili upate kukubarika... Paulo anasema👇
Wafilipi 4:5
[5]Upole wenu na ujulikane na watu wote. Bwana yu karibu.
Na zaidi anasema..
Wafilipi 2:14-15
[14]Yatendeni mambo yote pasipo manung’uniko wala mashindano,
[15]mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu,
((kwahiyo katika utendaji wako usitende mambo kwa manung'uniko au mashindano Bali wewe tenda mambo kwa usafi wa moyo kwa maana wewe waonekana kama Nuru kwa ulimwengu.
👉Na mwisho kijana ili usidhaurike hakikisha unaishi kwa upendo na tena unashikilia kwa ukamifu Imani ya Mungu wako hapo ndipo utaheshimika na jamii inayokuzuguka na zaidi hakikisha unakuwa msafi...Paulo anasema
Waefeso 5:3-4
[3]Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo wote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu;
[4]wala aibu wala maneno ya upuzi wala ubishi; hayo hayapendezi; bali afadhali kushukuru.
[[Ni Mimi kijana mwenzako katika Kristo Yesu
NAME: ZELLA MAJEMBE]]
Wafilipi 1:2
[2]Neema na iwe kwenu na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.
BARIKIWA.
Comments
Post a Comment