MUNGU AKUTIE NGUVU WEWE UNAYETAKA KUFANIKIWA KIROHO NA KIMWILI USIPITWE NA NENO HILI

 


MUNGU AKUTIE NGUVU WEWE UNAYETAKA KUFANIKIWA KIROHO NA KIMWILI USIPITWE NA NENO HILI.

(JIFUNZE KUWA MSIRI ILI UYAFIKIE MALENGO YAKO).

Utakuwa nami  sir. Majembe katika somo

Phone number +255757030926

BWANA YESU ASIFIWE!!k

kwanza kabla sijaendelea na somo lazima uelewe mafanikio Nini Nini?

👉tunasema MAFANIKIO ni ukamilishaji wa malengo yanayompatia mtu ustawi,hadhi na afya,Yaani mfano unaposema huu mwaka nitajenga nyuma na ukijenga huko ndo kufanikiwa,,


✓✓Sasa kwa sisi Wana wa Mungu Kuna kufanikiwa kiroho na kimwili...kufanikiwa kiroho ni kwa Mungu maana huku si kupenda kwetu Bali ni kwa Neema yake,yeye ndipo ametupa urithi wa kiroho ya kwamba tufanyike Wana..na kutukimiria ahadi nyingi zaidi..


2 Wakorintho 1:22

[22]naye ndiye aliyetutia muhuri akatupa arabuni ya Roho mioyoni mwetu. 


tena katika warumi anasema..""

Warumi 8:16-17

[16]Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu; 

[17]na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye. 


✓✓sasa Kuna mafanikio ya mwilini ambayo haya ni mahitaji yetu ya Kila siku lakini haya pia kuyapata na kuyatumiliza tunamhitaji Huyu Huyu Roho wa Mungu Ili atufanikishe,,kwamaana anasema


Yohana 3:8

[8]Upepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho. 

((kwahiyo uliye wa Mungu hakuna anayeweza kukutabiri zaidi ya Mungu,watakusikia tu kuwa umefanya ivi lakini hawatajua kuwa unataka kufanya Nini", tena ukishafanya ndipo watasikia))


NAMAANISHA IVI...""KUWA MSIRI

kwako wewe UNAYETAKA KUFANIKIWA ROHONI NA MWILINI,,siku zote shetani anatakiwa kuwa nyuma Yako na sio mbele Yako(Uwe msiri asiijue mipango Yako) yaani shetani anatakiwa awe anaona mafanikio Yako na sio mipango yako,, Kama wataka kufanikiwa hakikisha Hilo kwanza...""maana akiona mipango hakika atapambana na wewe sana na ndicho kitu tunachopitia wengi tume iweka sana mipango yetu wazi ivyo adui anajua Kila hatua tunayopiga(kwa lugha nyepesi uwe msiri kwa maana hata Roho mtakatifu husema nawewe tu,Wala jirani Yako hasikii kama umeambiwa jambo)


👉Na kinyume chake siku zote unatakiwa uhakikishe Mungu Yuko mbele yako,maana yeye ndiye hunyoosha mapito yetu...yaani mipango Yako Yote mshirikishe Mungu ,katika Mithali Neno linasema

Mithali 3:5-6

[5]Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, 

Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; 

[6]Katika njia zako zote mkiri yeye, 

Naye atayanyosha mapito yako. 

((Ivyo mpe Mungu uongozi wa akili na mawazo Yako...na katika Kila jambo muweke mbele,

kwa lugha nyepesi yote unayohitaji kiroho na kimwili Yako mikononi mwa Mungu...ila kama Baba kwa wale wanaotambua na kumuamini na kumpa tumaini lao..ndio hao Mungu huwapatia mahitaji Yao..maana anasema..


Mathayo 6:31-32

[31]Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini? 

[32]Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. 


👉kwahiyo katika kuhangaika kwako we mtafte kwanza Mungu Kisha mpe uongozi kwenye maisha yako ili ukiomba upewe..ukitenda ubarikiwe.. anasema ivi..

Mathayo 6:33

[33]Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. 


tena anasema ivi...

Kumbukumbu la Torati 28:1-3

[1]Itakuwa utakaposikia sauti ya BWANA, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo BWANA, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani; 

[2]na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya BWANA, Mungu wako.

[3]Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani. 

((nataka uelewe kitu hapa kiongozi yoyote hukaa mbele na sio nyuma...hata shule vilanja walikaa mbele Kisha wakatuamrisha mguu pande mguu sawa...nataka kusemaje...mtu pekee anayeweza kusikia sauti ya Mungu ni yule aliyemuweka Mungu kuwa Kiongozi wake Naam Huyu mtu ndiye mtu pekee atakayebarikiwa na akiitii sauti ya Mungu...Huyu ndiye atabarikiwa rohoni na mwilini.. katika efeso anasema👇


Waefeso 1:3

[3]Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo; 


NA ZAIDI MTU UNAYETAKA KUFANIKIWA JITAHIDI KUWA MSIRI,,

Mtu atasema kwanini??

👉Iko ivi mwana wa Mungu unapoongea shetani ndipo anajua mipango Yako(maana aliye nyuma hawezi jua mawazo ya mbele au kilicho mbele isipokuwa aliyepo mbele ndiye anajua,, kwahiyo wewe usipende kuwaambia watu mipango Yako, maana unakuta unamwambia unaezani ni rafiki Yako,ndipo kukatishwa tamaa kunaibuka,mara anakwambia hiyo biashara Ina hasara...mara sijui nani alifirisika...okay tufanye anaongea ukweli" lakini Kuna watu wanaifanya na wanastawi..how about them" ni Ivi ili ufike mbali...mpe Mungu mipango Yako na sio watu (shetani siku zote huibuka ndani ya mtu...kama ambavyo Mungu hutumia watu vivyo hivyo shetani naye hutumia watu...ko be careful!!


JIFUNZE HAPA

👉Yesu siku zote alikuwa hajawaambia wanafunzi wake kuwa imempasa kufa...ila Ile siku anawaambia imempasa kufa...shetani anaibuka ndani ya petro kuzuia kifo👇


Mathayo 16:21-23

[21]Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemu, na kupata mateso mengi kwa wazee na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka. 

[22]Petro akamchukua, akaanza kumkemea, akisema, Hasha, Bwana, hayo hayatakupata.

[23]Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu. 

((Yesu hakumkemea Petro Bali aliikemea Ile roho  ya kishetani iliyo kuwa imemvaa...anasema NENDA NYUMA YANGU EWE SHETANI..

👉HUU mstari una maana Pana sana na unatakiwa uju kama nilivyotangulia kusema..siku zote kwenye maisha yako Mungu ndiye anatakiwa awe Kiongozi yaani awe mbele Yako ili uyawaze ya mbele na shetani awe nyuma Yako laah! asikukaribie kabisa.." Ili asiyajue ya mbele Yako sasa bahati mbaya wengi wetu tumemuacha shetani ndiye anayeongoza maisha yetu kupitia marafiki zetu,ndugu zetu na majirani zetu...."" lakini wewe uliyepata Neema kuuona ujumbe huu..Basi jifunze leo kumpa Mungu Siri zako...maana yeye ndiye achunguzaye mioyo na viuno..👇


Yeremia 17:10

[10]Mimi, BWANA, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake. 

(means anayajua mawazo yetu na nia zetu...ni yeye pekee achunguzaye Wala hahitaji umuambie...kwahiyo weka Siri ndani Yako mshirikishe then atakusaidia na atakuinua.."


Wafilipi 1:2

[2]Neema na iwe kwenu na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo. 


BARIKIWA🙏🙏🙏

Comments